Fahamu historia fupi ya nguli wa soka, Pelè

0
40

Nguli wa soka  Edson Pelè (82) amefariki dunia leo Alhamisi Desemba 29, 2022 akiwa katika matibabu ya saratani ya katika Hospitali ya Albert Einstein huko São Paulo, Brazil.

Kupitia mtandao wa Instagram,  binti yake aitwaye Kely Nascimento amethibitisha kutokea kwa kifo chake.

Afya ya Pele ilikuwa ikizorota kadri alivyokuwa akizeeka. Madaktari  walisema mwishoni mwa Desemba kwamba alikuwa akipokea huduma ya kuharibika kwa figo na moyo kutokana na saratani aliyokuwa akipigana nayo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Pelė alikuwa mfungaji bora wa timu ya taifa ya Brazil akiwa na mabao 77 katika mechi 92 aliyocheza.

Edson Arantes do Nascimento alizaliwa Oktoba 23, 1940, alijulikana kama Pelé, jina la utani ambalo alidaiwa kujipatia baada ya kutamka vibaya jina la mwanasoka mwingine.

Pele alijiunga na Klabu ya Soka ya Santos huko Brazil mwaka 1956 akiwa na umri wa miaka 15 kama mshambuliaji.

Alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwaka mmoja baada ya kujiunga na Santos, kisha kucheza Kombe la Dunia mwaka uliofuata akiwa na umri wa miaka 17, akiwa mchezaji mdogo zaidi.

Alifunga magoli matatu (hattrick) kwenye nusu fainali dhidi ya Ufaransa na kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa fainali dhidi ya mwenyeji wa mashindano ya mwaka 1958, nchini Sweden.

Katika maisha yake ya kucheza Kombe la Dunia alifunga mabao 12 katika michezo 14 na anasalia kuwa mchezaji pekee wa soka kushinda kombe hilo mara tatu.

Katika maisha yake ya soka yaliyodumu kwa miaka 21 alifunga magoli 1,281 kwenye michezo 1,363.

Mchezo wake wa mwisho ulikuwa mechi ya maonesho kati ya Santos na Cosmos. Alicheza kipindi cha kwanza akiwa na Cosmos na kipindi cha pili akiwa na Santos.

Send this to a friend