Fahamu historia ya gari la bunduki lililotumika kubeba jeneza la Malkia na kwanini linavutwa na askari

0
44

Gari hili lilitumika pia kwenye mazishi ya wafalme wengine kadhaa wakiwemo King Edward VII, King George V na baba yake Malkia, King George VI, mnamo 1952.

Pia lilitumika katika mazishi ya Waziri Mkuu wa kwanza wa Malkia, Winston Churchill, na kutumiwa mara ya mwisho mnamo 1979 kwenye mazishi ya binamu yake Malkia, Lord Louis Mountbatten.

Utamaduni wa timu ya wanamaji wa Royal Navy kulivuta jeneza ulikuja baada ya farasi waliotumiwa kuvuta jeneza la Malkia Victoria mnamo 1901 kwenda kinyume na karibu kuinua jeneza lake.

Mnamo 1901, jeneza la Malkia Victoria lilipaswa kubebwa kwenye gari la bunduki katika mitaa ya Windsor. Hata hivyo katika baridi kali ya siku hiyo mwezi Februari, farasi waliokuwa wakilivuta waliingiwa na hofu na kujiinua huku wakitaka kuliangusha jeneza kutoka kwenye gari hilo.

Send this to a friend