Baadhi ya wanahistoria wanakadiria kwamba ya Siku ya Wajinga ilianza mwaka 1582 wakati ambapo Ufaransa ilibadili kalenda ya Julian na kuhamia kwenye kalenda ya Gregorian.
Kubadilika huku kwa kalenda kulibadilisha tarehe za mwaka na hivyo nchi hiyo ikaanza kusherehekea mwaka mpya Januari Mosi badala ya Aprili.
Lakini kwa bahati mbaya uamuzi huo uliyofanywa na Papa Gregory wa 13, haukuwafikia wananchi wote wa Ufaransa na badala yake baadhi wakaendelea kusherehekea mwaka mpya Aprili Mosi. Hivyo basi waliosherehekea mwaka mpya Aprili Mosi, waliitwa wajinga na siku hiyo ikaitwa ya wajinga.
Aina za magari bora zaidi kwa wanawake kuyatumia
Watu ambao walichelewa kupata habari au walishindwa kutambua kuwa mwanzo wa mwaka mpya ulikuwa umehamia Januari 1 na waliendelea kuusherehekea katika wiki ya mwisho ya Machi hadi Aprili 1 wakawa wanafanyiwa utani na wongo wakiitwa “Wajinga wa Aprili.”
Mizaha hiyo ilikuwa ni pamoja na kuwekewa karatasi zilizochongwa kwa muundo wa samaki migongoni mwao na akiitwa “poisson d’avril” (samaki wa Aprili), iliyosemekana kuashiria samaki wachanga, waliovuliwa kwa urahisi na mtu anayeweza kuhadaiwa kwa urahisi.
Siku ya wajinga duniani ilienea kote Uingereza wakati wa karne ya 18. Huko Scotland, ikiadhamishwa kwa watu kutumwa kufanya vitu au mambo yasiyowezekana na hata wengine kuwekewa mabango kama ya ‘nipige mgongoni’ au kuwekewa mikia bandia.