Fahamu kwanini unapata fangasi ya kucha 

0
107

Ni rahisi kupata maambukizi ya vimelea katika kucha, ikiwa una maambukizi ya vimelea kwenye mguu wako, fangasi inaweza kuenea na kusambaa kutoka kwenye kucha moja hadi nyingine.

Wataalam wanasema kwamba maambukizi ya kucha ni tatizo linalojitokeza zaidi kwa wanaume kuliko wanawake, na pia hutokea zaidi kwa watu wazima kuliko watoto. Kama una ndugu wa familia wanaougia sana tatizo hili, wewe pia upo hatarini kupata fangasi za kucha.

Endapo unapenda saluni kusafisha kucha zako, hakikisha unamkumbusha mhudumu kutakasa kwanza vifaa vyake. Hii itasaidia kupunguza hatari ya wewe kupata maambukizi ya fangasi kutoka kwa mtu mwingine.

Mambo ambayo yanaweza kuongeza hatari zaidi ya kupata fangasi ya kucha ni pamoja na:

•Umri mkubwa

•Kuvaa viatu vinavyofanya miguu yako kupata jasho sana

•Kutembea bila viatu katika maeneo ya umma yenye unyevunyevu, kama vile mabwawa ya kuogelea, sehemu za mazoezi na mabafu.

•Kupenda kuweka kucha bandia

•Kuwa na hali ya ngozi inayoathiri kucha, kama vile psoriasis

•Kuwa na ugonjwa wa kisukari, matatizo ya mtiririko wa damu au mfumo dhaifu wa kinga.

Mtu mwenye dalili ya fangasi ya kucha ni pamoja na sehemu ya kucha kugeuka kuwa rangi ya njano, kahawia, au rangi nyingine. Mara ya kwanza unaweza kuona doa tu katika kucha lakini kadri siku zinavyozidi Kwenda kucha hubadilika rangi. Bila matibabu, rangi hii inaweza kuenea kwenye kucha yako yote.

Pia kupinda kwa kucha, harufu mbaya kutoka kwenye kucha na kucha kuwa ngumu sana na nene.

Mambo ya kufanya kuepuka fangasi ya kucha ni pamoja na;

•Kuosha mikono yako baada ya kushika kucha iliyoathirika

•Kausha vidole vizuri baada ya kuoga hasa katikati ya vidole vya miguu

•Pata huduma za manicure na pedicure kutoka kwenye saluni ya kuaminika

•Epuka kutembea peku kwenye maeneo ya watu wengi

•Punguza matumizi ya kucha za bandia na rangi za kupaka kucha

Send this to a friend