Fahamu madhara ya kutumia maji kupoza injini ya gari

0
70

Moja ya makosa yanayofanywa na wamiliki wa magari ni kutumia maji kupoza injini. Maji ni rahisi kupatikana hivyo linapokuja suala la upoozaji wa injini maji yanakuwa chaguo la kwanza.

Wengi hawajui jinsi ‘radiator’ inavyofanya kazi na injini ya gari, ndiyo maana huwa wanakimbilia kutumia maji badala ya ‘coolant’(kimiminika kinachotumika kupoza injini). Kuna tofauti kubwa ya kutumia coolant na maji. Maji hupooza injini lakini hayafanyi kazi kama coolant inavyofanya.

Maji hupata joto haraka kuliko coolant. Joto husababisha hatari ya ‘injini block’ kupata ‘crack’ au kutanuka hasa endapo unatumia maji kwa safari ndefu. Block ikitanuka ‘piston rings’ hazitofanya kazi vizuri na gari litaanza kula oil.

Elimu muhimu kuhusu unywaji maziwa na umezaji dawa

Coolant imetengenezwa na viambata ambavyo vinalinda injini kupata kutu, lakini kutumia maji kuna sehemu za ndani za injini unazipa kutu kwa sababu injini imetengenezwa  na ‘cast iron’ ambayo inadhurika na kutu. Maji huleta tope ambalo baadaye litakwenda kuzungushwa kwenye radiator na kupelekea kuziba.

Ukitumia maji kwa muda mrefu water pump inawahi kufa sababu ya bearing [hazitaki maji] utasikia water pump inaanza kutoa kelele flani ukiwasha gari, ukisikia hivyo jua tayari ni tatizo.

Maji hayako kwa ajili ya kufanya upozaji wa injini ipasavyo hasa kwa injini zinazotumika muda mrefu na madhara yanayotokana na joto kwenye injini huwa ni gharama kushughulikia.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend