Fahamu magonjwa 8 yanayotibiwa kwa papai

0
60

Ulaji wa matunda si muhimu tu kwa ajili ya virutubisho mwilini, bali ni tiba inayosaidia kupambana na magonjwa mbalimbali.

Moja ya matunda yanayotajwa kuwa na faida kubwa kwenye mwili wa binadamu ni papai ambalo lina virutubisho vingi kama vile kalori, wanga, nyuzinyuzi, protini, vitamini C, vitamini A, vitamini B9, potasiamu, kalsiamu na magnesiamu.

Hizi ni faida za kula papai mara kwa mara;

Huzuia Saratani
Papai lina wingi wa vitu vya kuzuia saratani ikiwa ni pamoja na folate, vitamini C, beta-carotene na vitamini E ambayo hupunguza hatari ya saratani. Utafiti unaonesha kuwa ‘lycopene’ iliyomo kwenye papai inaweza kupunguza hatari ya saratani, pia linaweza kuwa muhimu kwa watu wanaopata matibabu ya saratani.

Cholesterol na Afya ya Moyo
Tafiti zimeonesha kuwa matunda na mbomboga zenye ‘lycopene na Vitamin C zinaweza kuzuia magonjwa ya moyo. Antioxidants zinazopatikana kwenye papai hulinda mishipa ya moyo dhidi ya kuziba kwa cholesterol na kusababisha mshtuko wa moyo.

Mtoto wa jicho
Papai limeonekana kupunguza hatari ya mtoto wa jicho. Papai lina wingi wa Vitamin A na beta-carotene ambazo ni muhimu kwa afya ya macho na uwezo wa kuona. Papai na karoti ni vyakula viwili ambavyo vimekubaliwa kuyapa macho afya kamili.

Maumivu ya hedhi
Papai ni miongoni mwa vyakula vinavyotumika kutuliza maumivu ya hedhi, kwa vile papai huwa na kitu kinachojulikana kwa jina la “papain” ambacho kinahusiana na damu ya hedhi, imeonekana kuchangia katika kurekebisha na kuboresha hali ya hedhi.

Gesi na Ukosefu wa Chakula
Papai hupunguza asidi tumboni, ikiwa mtu ana kiungulia na maumivu ya tumbo, papai ni tiba. Papai pia inasaidia katika usagaji wa chakula.

Mambo 6 hatari unayofanya kila siku

Afya ya Ngozi na Nywele
Papai hung’arisha ngozi na kukuza nywele kutokana na wingi wa vitamin A iliyomo na kuamsha tezi za mafuta mwilini na nywele, pia papai hupunguza chunusi ndio maana baadhi ya makampuni hupendelea zaidi ‘krimu’ au losheni za ngozi ambazo zimetengenezwa au zenye papai.

Pumu
Papai ni moja ya vyakula vinavyopunguza hatari ya pumu kwa sababu lina beta-carotene nyingi. Ikiwa una pumu, jaribu kula papai.

Afya ya Mifupa
Papai huongeza ufyonzaji wa kalsiamu kutoka kwenye mifupa, hupunguza utolewaji wa kalsiamu na figo na huwa na protini zinazolinda mifupa, ambazo zote kwa pamoja husababisha mifupa yenye afya.

Chanzo: BBC Swahili

Send this to a friend