Fahamu mambo manne yaliyojadiliwa kati ya Rais Samia na Rais wa Benki ya Dunia

0
35

Septemba 21, 2021 Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye yupo nchini Marekani kushiriki mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Dunia, David Malpass.

Katika mazungumzo yao wamejadili juu ya msaada wa Benki ya Dunia kwa Tanzania katika kukabiliana na athari za Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19) na kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo na ugonjwa huo. Rais Malpass amesema benki hiyo ipo tayari kusaidia ununuzi wa chanjo, kusafirisha na usambazaji kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa (International Development Association-IDA).

Pili, Malpass amepongeza jitihada za Tanzania kuimarisha mazingira ya kibiashara nchini, na kuwezesha ukuaji wa uchumi unaochangiwa na sekta binafsi kupitia mabadiliko ya taratibu za usimamizi.

Pia, amesisitiza umuhimu wa upatikanaji wa umeme, ujenzi wa nyumba nafuu na miundombinu ya kidijitali kupitia majawabu ya kikanda kukuza utendaji na masoko shindani.

Nne, viongozi hao walijadili kuhusu uwazi katika madeni, umakini katika kuchagua miradi ya uwekezaji na vyanzo vyake vya fedha.

Rais Samia anatarajiwa kuhutubia mkutano huo Septemba 23, 2021.

Send this to a friend