Fahamu sababu za kuongezwa kwa dakika nyingi kwenye michezo ya Kombe la Dunia nchini Qatar

0
53

Katika michezo mitatu iliyofanyika siku ya pili ya mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Qatar imekuwa na muda mrefu wa nyongeza.

Ushindi wa England wa 6-2 dhidi ya Iran ulikuwa na takriban dakika 30 za nyongeza katika vipindi vyote viwili kwa sababu ya majeraha ya kichwa kwa kipa Alireza Beiranvand na mlinzi Harry Maguire, pamoja na kutumia mud mrefu kutazama VAR.

Uholanzi walifaidika na jumla ya dakika nane zilizoongezwa katika kipindi cha pili cha ushindi wao dhidi ya Senegal huku wakifunga bao la pili, kisha mechi kati ya Marekani na Wales iliendelea kwa dakika tisa za ziada kwa sababu ya kusimama kwa kipindi cha pili.

Gwiji wa waamuzi wa Kamati ya Waamuzi FIFA, Pierluigi Collina amesema itakuwa jambo la kawaida kuona dakika nyingi za nyongeza katika mashindano ya mwaka huu.

“Fikiria mechi yenye mabao matatu, kushangilia kwa kawaida huchukua dakika moja, moja na nusu. Kwa hivyo ukiwa na mabao matatu, unapoteza dakika tano au sita. Tunachotaka kufanya ni kuhesabu kwa usahihi muda ulioongezwa, tulifanikiwa nchini Urusi [2018] na tunatarajia vivyo hivyo huko Qatar. Sizungumzii kuingilia kati kwa VAR, hii ni kitu ambacho ni tofauti na uhesabiwa na Refa msaidizi wa video kwa njia sahihi sana,” amesema.

Mechi zinazoshikilia rekodi kwa kusimama kwa muda mwingi zaidi ni katika mchezo mmoja wa Kombe la Dunia ambapo katika kipindi cha kwanza cha pambano la Uingereza na Iran kilikuwa na dakika 14 na sekunde nane, huku cha pili kikiwa na dakika 13 na sekunde nane.

Marekani dhidi ya Wales walikuwa na dakika 10 na sekunde 34 mwishoni mwa kipindi cha pili, na kipindi cha mwisho cha mechi kati ya Senegal na Uholanzi kwa dakika 10 na sekunde tatu.

Send this to a friend