FAHAMU TOFAUTI YA INFINIX HOT 12 NA SAMSUNG A13

0
63

 

Ni nini unapendelea Zaidi kwenye simu? Uwezo wa simu kuoperate kwa haraka au simu kwako ni camera?

Leo tunakuletea tofauti dhidi ya matoleo haya mawili Infinix HOT 12 na Samsung A13.
Kwanza, matoleo haya ni ya mwaka huu, Samsung ikiwa imetangulia kuingia sokoni na Infinix ikafuatia kuzinduliwa mwezi wa 4. Simu hizi zinafanana kwa baadhi ya features kama battery zote zikiwa na mAh5000 lakini zinaonekana kutofautiana katika vipengele hivi;

Samsung A13 ni simu yenye kamera nzuri ikiwa na Megapixel 50mp, 1.8wide + 5mp (ultrawide) + 2mp (macro) + 2(depth) macro main camera ambayo ni kamera kali sana.

Infinix kwa upande wa camera ikiwa imezidiwa na Samsung yenyewe ikiwa na 13mp + 1.8 wide + AF 2mp QVGA + 1080p@30fps na selfie camera ni MP8 matoleo hayo.
Infinix HOT 12 inatumia Chipset ya Mediatek G85 ni chipset yenye kasi katika kuchakata kazi hivyo kama ni mpenzi wa games au simu kwako ni ofisi basi hii ni chaguo sahihi kwa upande wa performance ya processor A13 inatumia Exynos 850 si processor mbaya ila hauezi kuilinganisha na speed ya processor ya HOT 12.

Simu hizi zinatofauti kubwa katika upande wa ujazaji simu chaji Infinix HOT 12 ina watt 18 na A13 ina watt 15 hivyo hot 12 inajaza charge kwa haraka Zaidi ukilinganisha na A13 na cha ziada katika swala la chaji Infinix HOT 12 inauwezo wa kudumu na chaji kwa masaa 2 endapo ikiwa na 5%.

Tofauti nyengine ni storage simu zote zinarom ya GB 128 zikitofautiana kwenye Ram Infinix ikikupa memory ya ziada ya GB 3 nakuifanya simu hii kuwa na Ram ya GB 7 na Samsung ikiwa na Ram ya GB 6 hivyo kwa HOT 12 mtumiaji anafasi ya kufungua files nyingi kwa wakati mmoja ukilinganisha na A13.

Simu zote zinamuonekano wa kuvutia isipokuwa Infinix HOT 12 design yake ni ya kisasa Zaidi eneo kubwa la mbele limetawaliwa na kioo kitaalamu muundo huu unafahamika kama Infinity Centred O Display ikiwa na inch 6.82 na A13 Design ya kioo ni water display cha inch 6.6 na vioo vyote ni IPS.

Upatikanaji zinapatikana katika maduka yote ya simu Infinix HOT 12 420,000Tsh na A13 500,000.

Send this to a friend