Fahamu undani wa kifo cha askari polisi shabiki wa Yanga

0
45

Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Mpwapwa mkoani Dodoma, Rashid Mohamed Juma ambaye ni shabiki wa Yanga alifariki dunia mwishoni mwa wili iliyopita wakati akitazama mchezo kati ya Simba na Yanga kupitia televisheni.

Rashid Mohamed Juma

Tukio hilo la aina yake limeibua hisia mbalimbali ambapo shuhuda aliyekuwa akitazama nae mpira amesema alifika dakika ya pili ya mchezo na dakika chache baadaye alianza kuishiwa nguvu.

“Alianza kuguna akiwa amesimama na nikamdaka baada ya kumlaza chini ndio akaendelea kuguna kama ng’ombe na kurusha mikono, baadaye akaguna mara ya mwisho na kunyoosha miguu na mikono,” amesema Joseph Ndani Mutalima

Ameongeza kuwa baada ya muda askari polisi walifika hapo na kumchukua, taarifa zilizofuata waliambiwa Rashid amefariki, na kifo hicho hakikutokana na goli la Yanga kama ilivyodaiwa, kwani wakati akiwa anajitapa tapa chini, ndio goli lilifungwa.

Mwili wa Rashid ambaye ameacha mjane na watoto wawili umepelekwa Rukwa kwa ajili ya mazishi.

Send this to a friend