Faida 10 za vitunguu maji mwilini

0
96

Matumizi ya vitunguu maji yanaweza kuwa ya kawaida kwenye mlo wako wa kila siku kutokana na kuwa kivutio kwenye chakula. Mbali na kukiongezea ladha chakula, kitunguu pia ni tiba na kinga nzuri kwenye mwili wa binadamu.

Hizi ni faida 10 za kiafya za matumizi ya vitunguu;

Kinga ya Magonjwa: Kitunguu kina ‘antioxidant’ nyingi ambayo husaidia kulinda seli za mwili dhidi ya uharibifu. Hii inaweza kusaidia kuzuia magonjwa mbalimbali kama vile saratani, ugonjwa wa moyo na kuzeeka mapema.

Hupambana na Bakteria: ‘Allicin’ katika vitunguu zinasaidia utumbo kupambana na bakteria hatari. Ndicho kiambato kinachosababisha harufu kali ya vitunguu na ndiye mpambanaji dhidi ya sumu na magonjwa.

Vitamini C: Je, wajua kuwa vitunguu vina kiasi kikubwa cha vitamini C? Vitamini C ni muhimu kwa mwili wako kufanya kazi vizuri. Inasaidia uundaji wa mishipa ya damu na kuboresha mfumo wako wa kinga.

Afya ya Mifupa: Kula vitunguu kunaweza kusaidia kuimarisha mifupa na kupunguza hatari ya kuvunjika kwa watu walio na umri zaidi ya miaka 50.

Kupunguza Uvimbe: Vitunguu vina ‘antioxidant’ inayoitwa ‘quercetin’. Quercetin hufanya kazi ya kupambana na uvimbe ndani ya mwili na kutibu maambukizi ya kibofu.

Nchi 10 za Afrika zenye matumizi makubwa ya bangi

Huboresha Usagaji Chakula: Vitunguu vina kiasi kikubwa cha ‘prebiotics na fiber’. Hii husaidia kuboresha afya ya utumbo kwa kusaidia katika usagaji chakula na kuimarisha mfumo wa kinga.

Afya ya Moyo: Kitunguu kinaweza kupunguza viwango vya cholesterol mbaya (LDL) na triglycerides kwenye damu, ambayo inaweza kusaidia kuzuia ugonjwa wa moyo.

Afya ya Utumbo: Kitunguu ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi ambazo ni muhimu kwa afya ya utumbo. Nyuzinyuzi husaidia kuboresha mmeng’enyo wa chakula na kuzuia matatizo ya utumbo kama vile kuvimba kwa utumbo na kufunga kwa choo.

Hupunguza Hatari ya Kisukari: Baadhi ya utafiti unaonyesha kuwa kitunguu kinaweza kusaidia kudhibiti viwango vya sukari kwenye damu na kuboresha usimamizi wa kisukari.

Afya ya Ngozi: Vitunguu vinaweza kusaidia kuboresha afya ya ngozi yako kutokana na ‘antioxidant’ iliyonayo. Inaweza kupunguza matatizo ya chunusi na kuongeza uzuri wa ngozi.

Send this to a friend