Faida 7 za kufanya ‘meditation’ asubuhi

0
92

Mazoezi ya kutafakari (meditation) kila asubuhi ni mojawapo ya mambo bora zaidi unayoweza kujifanyia. Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu wanaotafakari asubuhi wana furaha, afya, na mafanikio zaidi kuliko wale ambao hawafanyi hivyo.

Hizi ni faida saba za kufanya mazoezi ya kutafakari kila asubuhi;

1. Huboresha hali (mood) yako
Unapotafakari ndani ya dakika 15 itakusaidia kuongeza hisia chanya kama vile furaha, matumaini, hali ya amani na utulivu pamoja na umakini. Hivyo itakusaidia kuanza siku yako vizuri ukiwa mchangamfu.

2. Huongeza ufahamu wako
Kutafakari kila siku itasaidia kurahisisha kudhibiti mawazo hasi, na pia kujenga hali ya kuwa na shukrani kwa matukio mazuri unayopitia. Pia itakusaidia kujitambua zaidi na kuanza siku yako kwa ustadi na makini.

3. Hupunguza wasiwasi na kutuliza akili yako
Tafakari za asubuhi zinaweza kuleta utulivu mkubwa akilini mwako na kupunguza wasiwasi usio na sababu pamoja na mawazo. Kuanza siku yako ukiwa na utulivu italeta weledi katika kazi yako.

4. Inaboresha uzalishaji
Utaratibu wa kutafakari asubuhi utakuwezesha kukabiliana na majaribu na misukosuko unayopitia. Itakusaidia kupata majawabu kwa haraka na kwa ufanisi.

5. Huboresha afya na ustawi kwa ujumla
Kutafakari huboresha ustawi wako wa afya. Kwa mfano, inaweza kupunguza maumivu ya kichwa na kipandauso, husaidia shinikizo la damu na kukosa usingizi. Kupitia kutafakari, unaweza hata kuimarisha utendaji wa mfumo wako wa kinga na kupunguza maumivu ya kimwili.

Fahamu madhara yanayotokana na kunywa maji kupita kiasi

6. Huongeza kujiamini
Kupitia kutafari kila siku, kutajenga kujiamini na kuwa na mtazamo chanya na pia katika mazoezi yako kutakufanya kujitathamini na kujistahi.

7.Huongeza fadhili na huruma
Kutafakari kunapunguza viwango vyako vya mfadhaiko na kuongeza hali yako ya ufahamu wa kihisia. Inahimiza huruma zaidi na mtazamo mzuri pamoja na kujihusisha zaidi na watu wengine.