Faida kubwa 5 zinazotokana na Mradi wa Stigler's Gorge
Kwa mujibu wa Wizara ya Nishati, mradi wa Umeme wa Maji Rufiji (RHPP) ambao awali ulijulikana kwa jina laStiegler’s Gorge utakaozalisha umeme wa Megawati 2,115, unatarajiwa kuongezakasi ya ukuaji wa uchumi kwa Tanzania; nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasikatika Afrika Mashariki.
Utekelezaji wa mradi huu wa kihistoria unafuatia uamuzi mgumu na wenyekujali maslahi ya Tanzania ya sasa na ijayo uliofanywa na Serikali ya Awamu yaTano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kutekeleza ndoto iliyokaa bilakutimia kwa miaka zaidi ya 39 ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius KambarageNyerere. Tangu miaka ya 1970 hadi 1980, Serikali ya Mwalimu Nyerere ilijaribu kute-keleza mradi huu bila mafanikio.
Katika taarifa ya serikali ua uchambuzi wa mradi huo imeeleza kuwa, manufaa makuu ya mradi huu utakapoka-milika ni kupatikana kwa kituo na chanzokipya cha kuzalisha umeme kwakutumia nguvu za maji wa megawati 2,115ambao utaongeza chachu kwenye ukuajiwa uchumi na maendeleo ya kijamii.
Aidha manufaa mengine ni pamoja na:
- Kuzalisha ajira kwa Watanzania:Katika kipindi cha utekelezaji wa mradi,inakadiriwa wananchi 12,000 watapataajira za moja kwa moja na zile za kupitiautoaji wa huduma mbalimbali. Aidha,baada ya mradi kukamilika, inatarajiwa piakupatikana ajira za kudumu kwenye kituokipya cha uzalishaji wa umeme;
2. Bwawa Kuu litaongeza wigo wavivutio vya utalii kama vile kuanzishwa safari za boti, utalii wa uvuvi na upigajipi-cha majini;
3. Kubadilisha maisha ya wakazi wana-oishi ndani na nje ya eneo la mradi kupitia shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamiikama vile kilimo, uvuvi na kilimo chaumwagiliaji. Kwa miaka mingi wakazi waRufiji Chini wamekuwa wakiharibiwa mazao yao kwa mafuriko wakati wa mvua aukukosa maji ya kutosha wakati wa kiangazi.Ujenzi wa Bwawa Kuu utahakikisha maji yakutosha na kuwa kinga dhidi ya mafuriko nauhakika wa kupata maji mengi zaidi yatakayotiririka baada ya kutokakwenye mashine 9 za kuzalisha umeme iliwaendeleze shughuli za kilimo chaumwagiliaji;
4. Ujenzi wa Bwawa Kuu na uwepo waofisi za mradi kutaongeza ulinzi, uhifadhi wawanyama na kuzuia shughuli za ujangilikwenye eneo la Selous. Tayari shughuli zausanifu na maandalizi ya mradi na juhudinyingine za Serikali zimeanza kuongezaidadi ya tembo katika Pori la Selous; na
5. Faida ya moja kwa moja kwa Serikalini kupata mapato yatokanayo na ushuru waforodha na uuzaji wa umeme kwa wakan-darasi wakati wa utekelezaji wa mradi