Familia ya Mtanzania aliyeuawa vitani Ukraine imesema ilimzuia asiende vitani

0
50

Familia ya Mtanzania aliyeuawa katika vita nchini Ukraine, Nemes Tarimo (33) imedai ilimuonya kutokubali kupigana vita na vikosi vya Urusi nchini Ukraine, lakini kijana huyo alikuwa na motisha kubwa ya kujiunga.

Familia hiyo imesema Tarimo alikuwa Moscow akiwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Urusi, lakini alifungwa jela kwa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya, kisha baada ya muda alipatiwa taarifa za kujiunga na kundi la Wagner na kuahidiwa kuachiwa huru baada ya miezi sita ya kupambana kwenye vita.

Kijana huyo ambaye anatajwa na familia yake kuwa mpole, mwenye adabu na mcha Mungu aliwasiliana na familia yake mara ya mwisho mwezi Oktoba na kuwataarifu kuwa amekubali kujisajili kwenye kundi hilo.

‘’Alitupatia taarifa kuwa anajiunga kwenda kwenye vita dhidi ya Ukraine, tulimsihi sana asijiunge lakini akasema huwezi jua nitapata uhuru wangu kwa hiyo akajiunga, na mara ya mwisho kuwasiliana ilikuwa Oktoba 17 na hakupatikana tena.

Ndege tatu za ATCL zasimamishwa kuendelea na kazi

Baadaye tulipata habari mnamo Desemba kutoka kwa marafiki zake juu ya kifo chake,” ambacho kulingana na ripoti za vyombo vya habari, kilitokana na moto wa mizinga ya Ukraine.

Familia imesema inakusudia kumzika kijijini kwao Nyanda za Juu Kusini na kwamba hawawezi kufanya mpango wowote hadi watakapopokea mwili wake na kwamba inawauma sana kwani wamepoteza kijana aliyeheshimika sana.

Tukio hili linafanana na lile la kijana wa miaka 23 wa Zambia, Lemekhani Nyirenda ambaye pia alikuwa mfungwa nchini Urusi, na alifariki mwaka jana akiwa vitani na kundi la Wagner.

Send this to a friend