Familia yagomea polisi kufukua mwili unaodaiwa kuzikwa kimakosa

0
76

Jambo la kustaajabisha limetokea katika kitongoji cha Dungi, Kijiji cha Kibosho Kindi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya Polisi kushindwa kufukua mwili unaodaiwa kuzikwa kimakosa katika eneo hilo, huku ndugu wakidai hawana taarifa hiyo.

Mwili huo unaodaiwa kuwa wa Richard Shoo, aliyefariki dunia Juni 19, mwaka huu ulitakiwa kufukuliwa kwa ajili ya uchunguzi na vipimo vya vinasaba (DNA), baada ya familia moja kuibuka na kudai mwili uliozikwa si wa marehemu Shoo bali wa kijana wao, na mahakama iliamuru ufukuliwe kwa ajili ya taratibu za kisheria.

Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Moshi akiambatana na madaktari wawili, walifika eneo hilo kwa ajili ya kufukua mwili huo, lakini familia ilidai haijashirikishwa, hiyo waoneshwe kibali cha kufukua mwili huo ambacho polisi hawakuwa nacho.

Hata hivyo, Polisi walilazimika kuomba kutumiwa kibali hicho kwa simu ambacho walieleza walikiacha ofisini, lakini familia hiyo ilikataa na kudai wanahitaji kukiona, hali iliyosababisha kuahirishwa kwa shughuli hiyo.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend