Fanya haya kuzuia maumivu ya mgongo ukiendesha gari muda mrefu

0
65

Umiliki wa magari umeongezeka kwa watu wengi tofauti na miaka ya nyuma ambapo sasa watu wengi husafiri kwa kutumia magari yao binafsi katika safari ndefu.

Kuendesha gari kwa muda mrefu bila kupumzika kunaweza kusababisha madhara ikiwemo maumivu ya mgongo, hivyo ni muhimu kujiandaa vyema kwa kufanya mambo haya ili kuzuia maumivu:

Weka kiti vizuri
Weka kiti chako vizuri ili kuweka vizuri mkanda pasipo kuukaza sana ili uweze kuendesha gari kwa raha, kwa usalama na kuweza kuepuka maumivu ya mgongo, na ili kufanya hivyo, unapaswa kuzingatia hatua ambazo zitakusaidia kudhibiti kiti kulingana na mahitaji yako.

Zingatia mkao sahihi
Kuwa na umbali mzuri kati ya mwili wako na usukani ni muhimu ili usisumbue mgongo wako. Ili kupata mkao sahihi, unapaswa kuanza na miguu yako ambayo inapaswa kuwa kwa pembe inayofaa ili uweze kukanyaga mafuta ama kufunga breki kwa raha.

Zingatia urefu
Urefu ni muhimu pia, iwapo itabidi usumbue mgongo wako ili kutekeleza majukumu ya dereva, utakuwa na safari isiyo salama na uwezekano wa maumivu ya mgongo mwishoni. Urefu sahihi ni urefu ambao unaweza kuona kila kitu kwenye kioo cha mbele.

Epuka viboresha hewa
Epuka kuwa na ‘air freshener’ ndani ya gari kwa kuwa harufu hiyo inaweza kusababisha maumivu ya kichwa na itakufanya usijisikie vizuri ndani ya gari.

Chukua mapumziko
Ni muhimu pia kuchukua mapumziko mara kwa mara ili kunyoosha miguu yako, mikono na mgongo. Mapumziko yanapaswa kuchukuliwa kila kilomita 200 au kila saa mbili za kusafiri.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend