Miaka ya 20 ni wakati wa mapambano ya kuyaweka maisha yetu katika hali bora hapo baadaye. Nyakati hizi watu wengi hufanya makosa mengi lakini kubwa zaidi hutupa mafundisho na kutufanya kuwa imara.
Katika miaka hii kuna mengi unayopaswa kuzingatia na kujifunza ambayo yatakujenga kwa maisha yako yote, na haya ni baadhi ya mambo hayo;
1. Jenga utaratibu wa kulala saa 3 usiku na uwe macho saa 10 asubuhi kila siku. Masaa 7 ya usingizi ni kichocheo cha kuwa imara kwenye siku yako.
2. Kuwa na utaratibu wa kusoma, kuandika na kuorodhesha yale uliyoyaelewa kwa dakika 100 asubuhi.
3. Usiingie kwenye mahusiano na mtu mara baada ya kuachana na mtu mwingine, ukiwa katika hali mbaya au misukosuko. Rekebisha maisha yako kwanza.
4. Bila kujali kinachoendelea katika maisha yako, fanya kazi mara 7 kwa wiki. Ni tiba bora zaidi kwa afya yako ya akili.
5. Kuwa na kawaida ya kuoga maji ya baridi kila asubuhi. Inaponya mwili wako na kukutayarisha kwa siku mpya.
6. Usiache kutumia mtandao kama chanzo cha mapato yako. Kuna fursa nyingi za wewe kupata pesa.
Mambo 6 hatari unayofanya kila siku
7. Wajibika kwenye maisha yako kwa asilimia 100. Usiwalaumu wazazi wako, hali au mtu yeyote kwa masaibu yako.
8. Tembea angalau dakika 30 kwa siku kwenye jua. Kufanya hivyo kutasafisha akili yako, kutaboresha hali yako na kukufanya uwe mbunifu.
9. Hakikisha unazungukwa na watu walio na ari na ambao wanatamani sana kuboresha maisha yao. Mzunguko wako unapaswa kujadili zaidi kuhusu pesa, biashara na mafanikio.
10. Fanya asilimia 70 ya milo yako iwe protini. Itakusaidia kutengeneza, kujenga na kuimarisha mwili na akili yako.
11. Tambua kuwa ujuzi ni wa thamani zaidi. Jifunze ujuzi wowote ili kukusaidia kutatua matatizo ya kifedha katika nyakati mbalimbali.
12. Epukana na video za ngono na punyeto kwani ndio njia rahisi ya kuharibu maisha yako na muuaji mkuu wa mafanikio.
13. Kaa mbali na watu wanaokutumia kwa ajili ya maslahi yao, haijalishi wanamchango gani katika maisha yako, wao ndio kikwazo chako kikubwa cha mafanikio.