Fanya mambo haya 8 kuepuka saratani ya shingo ya kizazi

0
23

Saratani ya shingo ya kizazi ni aina ya saratani inayotokea katika sehemu ya chini ya mfuko wa uzazi au mlango wa kizazi. Saratani hii mara nyingi inahusishwa na maambukizi ya virusi vya papilloma (HPV), ambavyo ni kundi kubwa la virusi vinavyoenezwa kwa njia ya kujamiiana.

Ingawa si kila maambukizi ya HPV husababisha saratani ya shingo ya kizazi, inaweza kusababisha mabadiliko katika seli za shingo ya kizazi, ambayo baadaye yanaweza kusababisha saratani.

Dalili za awali za saratani ya shingo ya kizazi mara nyingi hazionekani, lakini kadri inavyoendelea, inaweza kusababisha dalili kama vile kutokwa damu wakati wa kujamiiana, kutokwa damu kati ya hedhi, maumivu wakati wa tendo la ndoa, au kutokwa na harufu mbaya.

Haya ni mambo nane ya kuzingatia kuepuka saratani ya shingo ya kizazi;

  1. Chanjo ya HPV: Kupata chanjo ya virusi vya papilloma (HPV) ni hatua muhimu ya kinga. Chanjo hutoa kinga dhidi ya aina muhimu za HPV zinazohusika na saratani ya shingo ya kizazi. Inashauriwa hasa kwa wasichana kuanzia umri wa miaka 9 hadi 26.
  2. Matumizi ya kondomu: Kutumia kondomu wakati wa kujamiiana husaidia kuzuia maambukizi ya HPV na magonjwa mengine ya zinaa.
  3. Lishe bora: Kula mlo kamili, ikiwa ni pamoja na matunda, mbogamboga, na nafaka nzima. Epuka vyakula vya kusindika, mafuta mengi na nyama nyekundu.
  4. Acha tumbaku: Kuacha au kutovuta sigara au matumizi ya tumbaku kunaweza kupunguza hatari ya kuendeleza kansa ya shingo ya kizazi.
  5. Punguza idadi ya wapenzi: Kudhibiti idadi ya wapenzi na kutumia kinga wakati kujamiiana, kunaweza kupunguza hatari ya maambukizi.
  6. Uchunguzi wa mara kwa mara: Kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara wa shingo ya kizazi ni muhimu kugundua mapema mabadiliko yoyote yanayoweza kusababisha kansa.
  7. Upuka ngono katika umri mdogo: Kushiriki ngono katika umri mdogo kunaweza kuongeza hatari ya maambukizi ya HPV.
  8. Shughuliksha mwili ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi dakika 30 angalau mara tano kwa wiki.
Send this to a friend