Fanya mambo haya matano kusahau kumbukumbu mbaya akilini mwako

0
71

Wakati fulani  kila mtu hupitia mambo ambayo asingependa kuyakumbuka. Hii inaweza kuwa kwa sababu ya hisia hasi kama vile woga, aibu, hatia, au huzuni ambayo tunaweza kuwa nayo.

Kwa bahati nzuri, kuna namna bora ya kufanya akili yako kukabiliana na kumbukumbu hasi na mwisho kuziondoa taratibu katika akili yako.

Hizi ni namna za kukabiliana na kumbukumbu usizozihitaji kichwani mwako;

 

1.Epuka vitu na maeneo ambayo yatakukumbusha kumbukumbu hasa

Sio vichochezi vyote vinaweza kuepukika kabisa lakini kuna baadhi unaweza kuviepuka. Kwa njia hii, kumbukumbu mbaya uliyonayo inaweza kuisha polepole.

Ni vizuri kuepuka maeneo yanayokukumbusha vitu ambavyo usingependa kuvikumbuka.

 

2. Zingatia zaidi kumbukumbu zenye furaha

Jaribu kuoanisha kumbukumbu yako mbaya na nzuri. Kwa mfano, ikiwa huwezi kuacha kufikiria wakati uliopigana na mtu wako wa karibu, basi unganisha kumbukumbu hiyo na kumbukumbu ya wakati ambao wote mliufurahia.

 

3. Ishi kulingana na wakati uliopo

Ikiwa una kumbukumbu mbaya zinazokusumbua, basi jitahidi kuzingatia wakati wa sasa badala ya kutumia muda na nguvu kubwa kuwa na hofu juu ya mambo ambayo huwezi kuyabadilisha. Kuzingatia wakati uliopo kutakusaidia kutabasamu kidogo na kujisikia vizuri.

 

4. Jiweke bize

Hakikisha unaweka ratiba ambayo itakupa muda mchache wa kukaa na kufikiria mawazo mabaya. Ikiwa unatabia ya kutumia muda mwingi peke yako, hakikisha kwamba unatoka zaidi na marafiki, au unatembelea familia yako mara nyingi zaidi.

 

5.  Usijipooze kwa dawa za kulevya au pombe

Kuzoea vitu vinavyobadilisha akili kunaweza kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, haswa ikiwa kumbukumbu mbaya imekuacha ukiwa na huzuni au wasiwasi. Unaweza kuishia kufanya mambo ya ajabu na mwisho ukayajutia.

Send this to a friend