Fatma Karume aondolewa kwenye orodha ya Mawakili Tanganyika

0
66

Kamati ya Maadili ya Mawakili Tanganyika imemkuta Fatma Karume na hatia ya kukiuka maadili ya Uwakili na hivyo imeamuru jina lake (Namba 848) kuondolewa moja kwa moja katika orodha ya mawakili nchini.

Umauzi huo umefikiwa leo na kikao cha kamati hiyo kilichokutana katika Mahakama Kuu ya Tanzania na kujiridhisha kuwa wakili huyo amekiuka maadili ya kada hiyo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Fatma Karume amesema hataukatia rufaa uamuzi huo.

Uamuzi wa kumuondoka kwenye orodha ya mawakili umekuja ikiwa ni siku mbili tangu kampuni ya uwakili, IMMMA Advocates aliyokuwa akiitumikia kumpa notisi ya kusitisha utumishi wake.

Septemba 2019, Jaji Kiongozi, Dkt. Eliezer Feleshi alimsimamisha kwa muda Karume kutokufanya shughuli za uwakili kutokana na kuwasilisha vielelezo visivyofaa na vyenye kufedhehesha kwenye kesi dhidi ya Rais Dkt. Magufuli na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi.

Send this to a friend