Fatma Karume: TFF ilipaswa kumtoza Fei Toto faini, si kumlazimisha abaki Yanga

0
30

Fatma Karume ambaye ni Mwanasheria wa mchezaji wa Klabu ya Yanga, Feisal Salum (Fei Toto) amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linamlazimisha mchezaji huyo kufanya kazi na Yanga wakati ni kinyume na sheria za FIFA.
Mwanasheria huyo amesema TFF ilipaswa kujiuliza ikiwa mchezaji huyo alivunja mkataba kwa njia sahihi au la, na kama hakutumia njia sahihi alipaswa apigwe faini na si kulazimishwa kuitumikia klabu hiyo.

“Sheria za FIFA zinasema kwamba ukivunja mkataba kinyume na makubaliano unapigwa faini, na unapigwa faini ili kuifidia timu na ili kuwafundisha wachezaji wengine wasifanye hivyo tena.

TFF yatupilia mbali shauri la Fei Toto

Kuna wakati fulani huwezi kuvunja mkataba kabla mkataba wako kumalizika, pia TFF walikuwa na haki kama wameona kavunja kwa wakati huo kusema usifanye kazi kwa miezi minne, lakini hawawezi kusema mkataba wake unaendelea,” amesema.

Aidha, amesema ikiwa mchezaji huo atasimamia msimamo wake wa kutoendelea kuichezea klabu hiyo, atamshauri aende katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Send this to a friend