FBI inachunguza nyaraka za siri zilizopatikana katika ofisi ya Rais Bidden

0
38

Idara ya Haki ya Marekani inachunguza nyaraka za siri zinazodaiwa kupatikana katika ofisi ya zamani ya Rais Joe Biden huko Washington DC.

Hati hizo zilipatikana karibu miezi mitatu baada ya Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI) kuvamia makazi ya Mar-a-Lago ya Rais wa zamani, Donald Trump na kukamata zaidi ya nyaraka 100 za siri za serikali huko Florida baada ya kumaliza muda wake.

Takribani mafaili 10 kati ya nyaraka hizo zilikutwa zimefungiwa mahali katika Kituo cha Penn Biden huko Washington mnamo Novemba na timu ya wanasheria ya Biden, na nyaraka hizo zimekabidhiwa katika Hifadhi ya Taifa.

Kulingana na wakili maalum wa Biden, Richard Sauber, kwamba faili hizo ziligunduliwa kabla ya uchaguzi na mawakili wa Biden ambao walikuwa wakihamisha vitu.

Brazil: Waandamanaji wavamia Bunge na makazi ya Rais, wachana nyaraka

“Ikulu ya White House inashirikiana na Hifadhi ya Taifa na Idara ya Haki kuhusu ugunduzi wa kile kinachoonekana kuwa rekodi za Utawala wa Obama-Biden, ikiwa ni pamoja na idadi ndogo ya nyaraka zilizo na alama za siri,” Richard Sauber, Wakili wa Rais Biden katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa CBS News, FBI inahusika katika uchunguzi wa nyaraka za siri zilizopatikana katika kituo hicho na Mwanasheria Mkuu wa Marekani Merrick Garland ametakiwa kupitia nyaraka hizo.

Send this to a friend