Fedha za UVIKO19 zawafukuzisha kazi Wakurugenzi wanne

0
38

Rais wa Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Wakurugenzi wanne wa Halmashauri kwa matumizi mabaya ya Fedha za miradi ya maendeleo hususani ni zile za Ustawi na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Wakurugenzi hao ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa Mkoani Mwanza, Manispaa ya Singida – Mkoani Singida, Halmashauri ya Jiji la Mbeya – Mkoani Mbeya na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mkoani Iringa.

Akizungumza mbele ya Rais, Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa amesema halmashauri zote ambazo zimetuhuniwa kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi uchunguzi umefanyika na kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita uchunguzi unaendelea.

Rais Samia ameagiza uchunguzi uendelee katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo napo kuna tuhuma za namna hiyo.

Send this to a friend