Fei Toto aomba kuchangiwa afungue kesi mahakama ya michezo (CAS)

0
50

Mchezaji wa Yanga, Feisal Salum (Fei Toto) ameomba msaada kwa Watanzania kumchangia pesa ili kufungua jalada la kesi kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) la kuvunja mkataba na klabu yake.

Feisal amesema TFF imeshindwa kumsaidia kupata haki yake ya kuvunja mkataba na klabu hiyo, hivyo ameamua kupeleka malalamiko yake CAS ambako anaamini huko atapata kile anachokihitaji.

“Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua kwenda Mahakama ya Michezo CAS,” amesema.

Kundi la Sauti Sol latangaza kutengana

Aidha, ameoneza kuwa “Nahitaji mchango wa kila Mtanzania mpenda haki na maendeleo ya wachezaji wa Kitanzania ambao wamekuwa kimya na woga juu ya maslahi, heshima na haki zao. Naomba unichangie kadiri utakavyoweza ili niweze kupata pesa ya kulipia gharama za kufungua jalada la kesi yangu CAS ili kupata haki yangu ya kuondoka Yanga kwa kuvunja mkataba,” amesema.

Hatua hiyo imekuja baada ya Feisal kuwasilisha barua kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ya kutaka kuvunja mkataba na klabu ya Yanga, ambapo kwa mara ya kwanza shauri hilo lilisikilizwa Januari 6 mwaka huu, na TFF ilitoa barua iliyoeleza kuwa Feisal bado ni mchezaji halali wa Yanga.

Send this to a friend