Mchezaji wa Yanga SC, Feisal Salum (Feo Toto) ameeleza matamanio yake ya kurudi uwanjani na kucheza mpira baada ya kukaa kwa muda mrefu akitafuta haki yake ya kuvunja mkataba na klabu yake.
Katika chapisho lake kwenye mtandao wa Instagram, Fei Toto ameandika kuwa amebakisha hatua chache ili kufanikisha nia yake ya kufungua mashitaka katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) hivyo amewaomba Watanzania kumchangia pesa na kufikia lengo lake.
“Ndugu zangu Watanzania, natamani kurudi uwanjani na kuendelea kuwafurahisha wapenda soka, nimebakisha hatua chache, nisaidieni niweze kukamilisha nia yangu ya kwenda CAS na kupata haki ya kurudi tena uwanjani.
Fei Toto aomba kuchangiwa afungue kesi mahakama ya michezo
Nimekumbuka Nyakati bora, nimekumbuka kupiga mashuti yangu ya mbali, nimekumbuka kufurahia na mashabiki wa soka. Fei Toto ni mmoja tu, msaidie arudi uwanjani kwa Haki inayotaka kudhulumiwa,” ameeleza.
Ombi la Feisal la kuvunja mkataba na Klabu ya Yanga lilikatiwa mara mbili kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji la Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na ndipo kutangaza kufungua jalada la kesi CAS akiamini huko atapata haki yake.