Fid Q: Wazazi ruhusuni watoto wa kike kuimba Hip Hop

0
34

Rapa maarufu kutoka Tanzania, Farid Kubanda (Fid Q) amesema ipo haja kwa Serikali kutoa elimu kwa wazazi ili watoto wa kike waruhusiwe kufanya muziki wa Hip hop.

Fid Q amesema amegundua uwezo mkubwa walionao wasanii wa kike katika muziki huo ambao jamii bado inauchukulia kama muziki wa kihuni.

“Tanzania tuna namba ndogo sana ya wasanii wa Hip Hop kuanzia wanawake na wanaume, na nilichokigundua watoto wa kike wakiimba Hip Hop huwa wanafanya vizuri sana, tatizo ni makatazo kutoka kwa wazazi wao.

Ndio maana nikashauri Serikali itoe elimu kwa wazazi ili watoto wa kike waruhusiwe,” amesema Fid Q.

Nyimbo 10 za Tanzania zinazotazamwa sana YouTube kuanzia mwezi Februari 2023

Ameongeza kuwa ikiwa hilo litafanyika basi anaamini litaongeza namba ya wasanii wa Hip Hop na muziki huo utakuwa kama ulivyo muziki wa Bongo Fleva na Taarabu.

Akitoa mifano ya wasanii wa kike wa muziki huo Rose Ree na Chemical, amesema ni baadhi ya wasanii ambao wana mashabiki wengi kutokana na nyimbo zao kuigusa jamii.

Send this to a friend