
Rais wa FIFA, Gianni Infantino amelaani kitendo cha baadhi ya wachezaji na benchi la ufundi la Senegal kuondoka uwanjani baada ya mwamuzi kuipa Morocco penati dakika za mwisho katika mchezo wa fainali wa AFCON.
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii, amesema kuwa kitendo hicho hakikubaliki huku akizitaka timu kuheshimu maamuzi ya waamuzi wa mechi.
Kwa bahati mbaya, pia tulishuhudia matukio yasiyokubalika uwanjani na kwenye viti vya mashabiki. Tunakemea kwa nguvu tabia ya baadhi ya “wafuasi” pamoja na baadhi ya wachezaji na benchi la ufudi la Senegal. Haikubaliki kuondoka uwanjani kwa namna hiyo, na vilevile, vurugu haiwezi kuvumiliwa katika mchezo wetu, kwa sababu si sahihi.
Daima lazima tuheshimu maamuzi ya waamuzi wa mechi ndani na nje ya uwanja. Timu lazima zishindane uwanjani na kufuata Sheria za Mchezo, kwani jambo lolote chini ya hili linaweka hatarini msingi wa mpira wa miguu,” amesema.
Aidha, amesema anatarajia kwamba vyombo husika vya kinidhamu vya CAF vitachukua hatua stahiki juu ya kitendo hicho.
Baadhi ya wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani, mchezaji Sadio Mané aliwashawishi wenzake kurejea uwanjani na kuendelea na mchezo.
Hatimaye, Morocco ilikosa penalti hiyo na kupoteza mchezo kwa kufungwa bao 1-0.







