FIFA yaifungia Biashara United

0
42

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeifungia kusajili klabu ya Biashara United mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake, Tayo Odongo.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesema uamuzi huo umefanyika baada ya mchezaji huyo kufungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na kushinda kesi hiyo dhidi ya klabu.

“Klabu hiyo ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45, tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini haikutekeleza uamuzi huo,” imeeleza TFF.

Baada ya FIFA kuifungia kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, TFF imeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa ndani.

Send this to a friend