FIFA yaifungia Simba kusajili

0
56

Klabu ya Simba imefungiwa kusajili wachezaji mpaka itakapolipa madai ya klabu ya Teungueth ya nchini Senegal inayodai sehemu ya malipo kutokana na mauzo ya aliyekuwa mchezaji wao, Pape Ousmane Sakho.

Kwaa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya klabu hiyo kushinda kesi ya madai dhidi ya Simba kuhusu madai ya mchezaji huyo ambaye hivi sasa anachezea timu ya Quevilly Rouen Metropole ya nchini Ufaransa.

“Simba ilitakiwa iwe imetekeleza uamuzi huo ndani ya siku 45 tangu ulipotolewa, lakini haikufanya hivyo,” imesema taarifa iliyotolewa na TFF.

Kufuatia uamuzi wa FIFA, TFF imeifungia Simba SC kufanya uhamisho wa ndani na kuzikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni, sheria na taratibu za mpira wa miguu ili kuepusha adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa.

Send this to a friend