FIFA yazifungia Fountain Gate na Kitayosce kusajili

0
49

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limezifungia klabu za Kitayosce iliyoko ligi kuu ya NBC na Fountain Gate inayocheza ligi ya Championship kusajili wachezaji.

Uamuzi huo umefanyika baada ya kocha raia wa Misri aliyewahi kuzifundisha timu hizo kwa nyakati tofauti, Ahmed El Faramawy  Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hizo akipinga kuvunjiwa mikataba kinyume cha taratibu.

“Baada ya Soliman kushinda kesi, klabu hizo zilitakiwa ziwe zimemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini hakuzitekeleza hukumu hizo,” imesema taarifa illiyotolewa na TFF.

Je! wakati sasa CAF ifute ushindi wa goli la ugenini?

Aidha, kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) imezifungia kufanya usajili wa ndani.

Send this to a friend