Filamu 5 kali za kuangalia wikiendi hii

0
36

Ikiwa wewe ni mpenzi wa filamu basi hapa ni mahala pake, leo tunakuletea filamu 5 bomba ambazo zimetoka hivi karibuni zitakazochangamsha wikiendi yako na kukupa burudani unayoihitaji;

Secret Invasion
Nick Fury anajifunza juu ya uvamizi wa kisiri wa dunia na kikundi cha Skrulls wanaobadilisha sura. Fury anaungana na washirika wake, ikiwa ni pamoja na Everett Ross, Maria Hill na Skrull Talos, na kurudi duniani kukamilisha misheni yao ambayo haijakamilika.

Strength of woman
Kendra ambaye anajikuta katika matatizo na ndoa yake analazimika kufanya maamuzi kwa ajili ya maisha yake. Ben anaporudi maishani mwake bila kutarajia anampa nguvu ya kukabiliana na maisha yake yenye changamoto na kisha kukubali upendo ambao Ben anampatia.

Kandahar
Huko Kandahar, Tom Harris (Gerard Butler), mfanyakazi wa siri wa CIA, amekwama katika eneo hatari nchini Afghanistan. Baada ya misheni yake kufichuliwa, inamlazimu apambane ili aweze kutoka pamoja na mtafsiri wake wa Afghanistan hadi eneo la Kandahar, huku akiepuka majeshi ya adui na wapelelezi waliopewa jukumu la kuwawinda.

Meet me in Paris
Ni filamu ya wanawake watatu kutoka Marekani ambao wanasafirishwa kwa ndege hadi Paris na kukaa katika nyumba ya kifahari kwa siku 10 huku wakijaribu kutafuta mapenzi ya kweli au kufurahia walau kidogo kabla ya kurudi nyumbani.

Gumraah
Filamu hii inawahusisha ndugu wawili mapacha ambao mmoja wao anafanya uhalifu wa mauaji na baadaye kuwapa wakati mgumu polisi baada ya kutumia mbinu zinazowaweka katika nyakati ngumu.

Send this to a friend