Filamu 5 kali za kuangalia wikiendi hii

0
44

Unafahamu filamu kali zilizotoka hivi karibuni? Huhitaji kufikiria zaidi, kwani hapa kuna filamu mpya na bora zitakazoichangamsha wikendi yako.

Bird Box Barcelona
Baada ya nguvu ya ajabu inayoangamiza idadi ya watu wengi duniani, Sebastian na binti yake wanajaribu kujiokoa kutoka kwa viumbe vya ajabu visivyoonekana.

Mtu yeyote anayeona nguvu hiyo ya kutisha, mara moja anaangamizwa. Baadhi wanawachukulia viumbe wauaji kama malaika, na kuwalazimisha wengine kuwatazama ili “kuokoa” roho zao.

The Little Mermaid
Ni hadithi nzuri ya Ariel, nguva mrembo na mdogo zaidi kati ya binti za Mfalme Triton. Ariel anatamani kujua zaidi juu ya ulimwengu ng’ambo ya bahari, anajikuta akimpenda Prince Eric na kufanya makubaliano na mchawi wa bahari ili apate nafasi ya kuishi nchi kavu na hatimaye anayaweka maisha yake na taji la baba yake hatarini.

Hidden Strike
Wanajeshi wawili wa zamani wa vikosi maalum Cena na Chan wanadhamira ya kuwalinda raia wanaposafiri kwenye barabara hatari inayoitwa “Barabara kuu ya Kifo” huko Baghdad ili kuwafikisha mahali salama panapoitwa Green Zone. Wakati wa safari yao, wanakabiliwa na changamoto nyingi na matukio ya kusisimua.

The Cloned Tyrone
Fontaine, mfanyabiashara wa dawa za kulevya anapigwa risasi na mpinzani wake Isaac na kupata mshtuko anapoamka asubuhi bila kuwa na majeraha. Yeye na Slick Charles na Yo-Yo wanaanza kuchunguza tukio hilo. Utafutaji wao hatimaye unawapeleka kwenye eneo kubwa la chini ya ardhi ambapo kuna maabara inayoungwa mkono na serikali inafanya majaribio kwa watu weusi wa eneo hilo.

Joy Ride
Filamu hii inaawahusu marafiki wanne wanapoungana na kugundua maana halisi ya kujijua na kujipenda kwa jinsi walivyo, huku wakisafiri sehemu mbalimbali kumtafuta mama wa mmoja wao ambaye hakuwahi kukutana naye.

Send this to a friend