Filamu 5 kali za kuangalia wikiendi hii

0
42

Unafahamu filamu kali zilizotoka hivi karibuni? Huhitaji kufikiria zaidi, kwani hapa kuna filamu mpya na kali zitakazokupa utulivu na kufurahia wikendi yako.

No Hard Feelings

Maddie (Jeniffer Lawrence) anafikiri kuwa amepata suluhisho la matatizo yake ya kifedha baada ya kupata kazi inayovutia. Wazazi matajiri wanamchagua Meddie kutoka kimapenzi  na mtoto wao wa miaka 19 mwenye aibu, Percy  ili kuongeza kujiamini kwake kabla ya kuondoka kwenda chuo kikuu. Lakini kwa bahati mbaya mapokeo ya kijana huyo yanakuwa tofauti na matarajio ya Meddie.

Cobweb

Peter mwenye umri wa miaka nane na asiye na marafiki shuleni. Mara kwa mara anaamshwa na sauti mithiri ya mtu anayegonga ukuta wa chumba chake huku wazazi wake wakipuuza kuwa yote ni mawazo yake. Peter anaendelea kuzungumza na mtu wa ajabu ambaye anajitambulisha kuwa anaitwa Sara na kudai alifungiwa ndani ya ukuta na wazazi wa Peter. Mtoto huyo anaamini kuwa wazazi wake wanaweza kuwa wanaficha siri mbaya na ya hatari.

Hidden Strike

wanajeshi wawili wa zamani  John Cena na Jackie Chan wa vikosi maalum wanakabiliwa na jukumu la kusafirisha kikundi cha raia wasio na hatia kupitia barabara hatari zaidi ulimwenguni huku wakikabiliwa na vikwazo vya kijeshi na hatari za kila aina, wanajeshi hawa wa zamani wanalazimika kuungana na kutumia ujuzi wao wote kuwalinda raia hao na kuwapeleka salama kwenye eneo lenye usalama.

Spider-Man: Across the Spider-Verse

Baada ya kukutana tena na Gwen Stacy, Spider-Man wa Brooklyn anarushwa kwenye maeneo tofauti ya ulimwengu, ambapo anakuta kikundi cha watu wa kipekee wanaojulikana kama “Spider-People” ambao wanajukumu la kulinda ulimwengu huo. Miles anajikuta akipigana na kikundi hicho na kulazimika kubadilisha maana ya kuwa shujaa ili aweze kuwaokoa watu anaowapenda sana.

Heart of Stone

Wakala wa kimataifa wa kijasusi, Rachel Stone ana jukumu la hatari la kulinda amani katika shirika lake la kimataifa la kulinda amani ambapo anajikuta anapoteza mali yake ya thamani zaidi iliyopewa jina la siri la Moyo. Anajitahidi kupambana ili kuiokoa mali hiyo kutoka kwenye mikono ya maadui.

 

Send this to a friend