Filamu 5 kali za kutazama wikendi hii

0
57

Unafahamu filamu kali zilizotoka hivi karibuni? Huhitaji kufikiria zaidi, kwani hapa kuna filamu mpya na kali zitakazokupa utulivu na kufurahia wikendi yako.

The Engineer
Wakati Israel imekumbwa na mlolongo wa milipuko ya kigaidi, binti wa seneta wa Marekani anakufa katika mojawapo ya milipuko hiyo. Sasa, Etan (Hirsch), analazimika kuongoza kikosi maalum cha wakala na wapiganaji wa siri ili kumtafuta mtu anayehusika na matukio hayo.

Inside Man
Mpelelezi wa polisi aliyeharibiwa sifa yake na kufukuzwa kazi, anataka kurejesha heshima yake kwa kuingia kwa siri katika genge la uhalifu lenye ghasia. Lengo lake ni kufichua shughuli za kiuhalifu za genge hilo na kuleta haki kwa kufichua ukweli. Hata hivyo, wakati anavyozidi kuchimba ndani ya shughuli za kundi hilo la uhalifu, anagundua kuwa mambo si rahisi kama alivyodhani.

Pretty Crazy
Kijana aliyefanikiwa na mtanashati anaamua kutafuta mtu wa kutulia naye na kujenga naye maisha pamoja. Baada ya uhusiano wake wa mwisho, anakutana na kumpenda msichana wa ndoto yake, lakini je, maisha yake ya nyuma yatarudi kuharibu nafasi ya kujenga maisha yake pamoja na binti huyo? Fuatilia filamu hii ya kuvutia.

Kill Shot
Kiongozi wa uwindaji na mteja wake mpya anayeoneka kuwa na siri nyingi, wanakutana na dola milioni 100 kwenye vifusi vya ajali ya ndege, lakini furaha yao inapotea ghafla baada ya kugundua kuna kikundi cha watu kinawafuatilia ambacho kimetumwa kurejesha fedha hizo. Lazima wapigane ili kujinasua kutoka eneo lenye adui wakali.

Greatest Days
Filamu hii ni kuhusu marafiki watano ambao wanapata fursa ya kufurahia usiku wa kusisimua wanapohudhuria tamasha la bendi yao wanayoipenda sana. Baada ya miaka ishirini na tano, wanakutana tena kwenye bendi hiyo huku maisha yao yakiwa yamebadilika, lakini kitu kimoja kinachowaunganisha ni upendo wao kwa bendi ileile wanayoipenda.

Send this to a friend