Filamu 5 kali za kutazama wikiendi hii

0
40

Kuangalia filamu ni kati ya burudani nzuri inayoweza kukupa utulivu hasa filamu hiyo ikiwa ni ya kuvutia.

Unaweza kutumia muda wako wikiendi hii kutazama filamu hizi mpya na kali ukiwa na marafiki au hata peke yako;

  1. Aloha heart

Sarah ambaye ni binti mchapakazi anaamua kuchukua mapumziko ya wiki moja kwa ajili ya harusi ya rafiki yake mkubwa huko Hawaii. Huko anakutana na  Manu  ambaye ni meneja mpya wa hoteli na kumsaidia kufanya mabadiliko kwenye hoteli hiyo ya wazazi wake, lakini wanajikuta wanaanzisha safari nyingine ya mahusiano.

Big Nunu’s Little Heist

Mwanajeshi wa zamani anaburutwa kwenye genge la wahalifu wa eneo hilo ili kuondoa wizi katika kitongoji maarufu cha Afrika Kusini.

Hadithi hii ya kuchekesha ya kundi la wafanyakazi wa kiwandani na majambazi wenye ndoto ya mambo makubwa, wanaiba bunduki na kisha kuiba kiasi kikubwa cha pesa.

Fear The Night

Wanawake wanane wanakusanyika kwa ajili ya sherehe ya kumtakia heri ya ndoa mwenzao katika nyumba iliyoko milimani California. Lakini mapumziko yao yanatiwa doa baada ya wageni walioficha nyuso zao kuwavamia na kuzunguka eneo hilo na kuanza kurusha mishale kuelekea katika nyumba yao.

Sasa jukumu la kuongoza wanawake katika kupambana na kutetea usalama wao na kujiokoa usiku huo linawekwa mikononi mwa Tess, mwanamke mwenye uzoefu wa kijeshi. Je, wataweza kuokoa maisha yao na kushinda usiku huu wa kutisha?

Insidious: The Red Door

Josh Lambert anaenda mashariki kumpeleka mwanae, Dalton chuoni. Hata hivyo, ndoto ya kujiunga chuo kikuu ya Dalton inabadilika kuwa janga la kutisha wakati pepo zilizofichwa za kale, ghafla zinarudi kumtesa yeye na baba yake. Wanajaribu kukabiliana na vitisho vilivyojificha ili kujiokoa.

River Wild

Ndugu wawili ambao wanapendana lakini hawaaminiani wanaanza safari kwaajili ya michezo ya majini kwa kutumia mtumbwi pamoja na kikundi kidogo cha watalii. Rafiki yao wa utotoni ambaye alialikwa, anajitokeza kuwa hatari zaidi kuliko walivyodhani.

Safari ya kusisimua inabadilika haraka na kuwa ya kutisha, wakati wote wakiwa kwenye mtumbwi wanajikuta wakipigania maisha yao huku mtu anayeonekana kuwa na nia mbaya akijaribu kuhakikisha siri za kushangaza zinabaki kuwa siri.

 

Send this to a friend