Filamu 5 za kali za kuangalia wikendi hii

0
45

Je, ratiba yako ya filamu wikendi hii ikoje? Kama bado hujui ni filamu gani nzuri ungalie basi usihofu, hizi ni filamu 5 mpya ambazo zitakufaa wikendi hii;
1. Hijack
Hijack ni filamu yenye msisimko wa hali ya juu inayohusu safari ya ndege iliyotekwa nyara wakati ikielekea London katika safari ya saa saba, huku mamlaka za ardhini zikihangaika kutafuta majibu.
Idris Elba aliyeigiza kama Sam Nelson mfanyabiashara mkubwa duniani anajikuta mmoja kati ya walionaswa kwenye ndege hiyo ambapo anapambana kuokoa watu kutoka kwa watekaji.

2. The Covenant
Mkalimani wa Afghanistan Ahmed Anamfuata Sajenti wa Jeshi la Marekani, John Kinley kuokoa maisha yake. Ahmed anahatarisha maisha yake mwenyewe kumbeba John aliyejeruhiwa ili kumpeleka mahali salama kabla ya Taliban kuwawinda.

3. Knights of the Zodiac
kijana shupavu wa mitaani, anatumia muda wake kupigania pesa huku akimtafuta dada yake aliyetekwa nyara. Anagundua nguvu za ajabu ambazo hakujua kamwe alikuwa nazo. Seiya anajikuta akiingizwa katika ulimwengu wa watakatifu wanaopigana huku akipewa mafunzo ya kale ya kichawi na mungu wa kike.

4. Daughter of the bride
Diane na Kate ambao sio mama na binti pekee bali pia marafiki bora, Kate anadhani mama yake anahitaji mwenza kutokana na kukaa peke yake kwenye nyumba kubwa. Anakutana na Bruce ambaye anadhani atamfaa mama yake na kumpa namba ya simu ya mama yake kwa siri.

5. Mavka: The Forest Song
Mavka anakabiliwa na chaguo kati ya mapenzi na jukumu lake kama mlezi wa moyo wa msitu, anaanguka katika mapenzi na mwanadamu ambaye ni mwanamuziki mchanga mwenye talanta, Lukas aliyetaka kumponya mjomba wake anayehitaji mti wa uzima.

Send this to a friend