Filamu 7 mpya za kutazama wikiendi hii

0
61

Ikiwa unajiuliza ufanye nini wikiendi hii, basi unaweza kuchagua kutazama filamu bora na za kusisimua zilizotoka mwezi Mei, mwaka huu.

Hizi ni filamu sita za kutazama ambazo zitachanyamsha wikiendi yako;

Love Again
Ikiwa hujaitazama muvi hii, basi wikendi hii inaweza kuwa bora zaidi kama utaitazama pamoja na wapendwa wako.

Filamu hii inamhusu mwanamke aliyefiwa na mchumba wake, hivyo anajaribu kupunguza uchungu wa kifo chake kwa kutuma ujumbe wa kimapenzi kwa namba ya zamani ya simu ya mchumba wake bila kujua kuwa anatuma ujumbe kwa mwanaume ambaye amepewa namba hiyo kuitumia.

Fast X
Filamu hii ni toleo la kumi la Fast and Furious katika muongo wake wa tatu. Toretto (Vin Diesel) na familia yake wamefanya kila namna kumshinda adui, na sasa wanakabiliana na mpinzani mbaya zaidi ambaye hawajawahi kukutana naye mwenye kisasi cha damu, na ambaye ameazimia kusambaratisha familia hiyo, pamoja na kuharibu kila kitu na kila mtu ambaye Dom anampenda.

The Mother
Filamu ya  ‘The Mother’ Inamhusu mfanyakazi wa zamani wa jeshi la Marekani (Jennifer Lopez) ambaye anashirikiana na wakala wa FBI kumwokoa binti yake baada ya kutekwa nyara na wahalifu. Anatokea mafichoni baada ya kuachana naye miaka ya nyuma wakati akikimbia kutoka kwa wanaume hatari.

Extraction 2
Baada ya kunusurika kifo katika matukio ya filamu ya kwanza, Rake amerejea kama askari mwenye nguvu mpya akiendeleza jukumu alilopewa la kumwokoa mtoto anayetokea katika familia ya kitajiri ambaye ameshikiliwa na kikundi cha majambazi katili. Mapambano yanakuwa makali na yenye misukosuko kuhakikisha anatimiza misheni yake.

John Wicky
John Wick (Keanu Reeves) anafichua njia ya kuwashinda maadui zake. Lakini kabla ya kupata uhuru wake, Wick lazima akabiliane na adui mpya aliye na nguvu zinazogeuza marafiki wa zamani kuwa maadui.

Moon gardener
Filamu hii inamhusu mtoto mdogo ambaye familia yake haiishi mabishano. Anapoteza fahamu baada ya kuanguka, na anapokuwa nje ya fahamu zake anashindana na jinamizi linalomtesa, huku akijaribu kufanya kila njia kutafuta njia ya kurudi katika fahamu zake.

The Little Mermaid
Hii ni filamu inayomhusu nguva mrembo, mkaidi na mdogo zaidi kati ya binti wa mfalme Triton. Ariel anatamani kujua zaidi kuhusu nchi kavu, na wakati alipotembelea anajikuta akimpenda Prince Eric baada ya kumwokoa.

Ingawa nguva ni marufuku kuingiliana na wanadamu, Ariel anafuata moyo wake. Anafanya makubaliano na mchawi hatari wa baharini, Ursula na kupata nafasi ya kufurahia maisha ardhini na  hatimaye kuweka maisha yake  na taji la baba yake hatarini.

Send this to a friend