Filamu (Movies) 24 unazopaswa kuzitazama kabla hujafikisha miaka 30

0
9

The Breakfast Club (1985)

Ni filamu ya nyuma kidogo. Lakini hata kama tayari umepita umri wako wa shule, bado filamu hii ina maana sana kwako  kwani mihangaiko na mapambano yanayooneshwa na waigizaji yanakufunza kuwa kwenye maisha kila mtu anapambana na hakuna ambaye mambo yanamjia kirahisi.

The Silence of the Lambs (1991)

Filamu hii ilinifunza kwamba, kama mwanamke, nina uwezo wa kufanya chochote kile kinachofanywa na mwanamume. Pia ilinifunza kwamba, kila kitu hakipo kama kinavyoonekana na kwamba, Imani ni kitu kikubwa sana, sio cha kuweka kwa mtu yeyote.

Eternal Sunshine of the Spotless Mind (2004)

Kwa wale wapenzi wa filamu za mahusiano, nadhani sina ya kundika maneno mengi, tafuta muda wako, tazama filamu hii, halafu urudi unishukuru.

Dead Poets Society (1989)

Katika maisha, unapaswa kusimama kwa ajili yako badala ya kusubiri mtu wa kukutetea aje. Na unaposimama una wajibu wa kuwahoji wazazi, walimu na wengine wote wale ambao unaona wana fanya vitu kinyume na mtazamo wako, badala ya kutii tu kila unachoambiwa.

Clueless (1995)

Itazame

Into the Wild (2007)

Ni sawa kugeuka nyuma, kuomba msaada na kukiri kwamba umeshindwa.

Once (2007)

Stori ya kusisimu ya mapenzi kupitia muziki. Mastaa wa filamu hiyo pia ndio walitunga nyimbo hizo, ji filamu ya kusisimua.

Blue Valentine (2010)

Filamu hii itakuandaa endapo mambo katika uhusiano ulionao yatakwenda mrama.

The Goones (1985)

Wakati wote ifuate ramani ya hazina unaweza kupata dhahabu.

Now and Then (2010)

Hasa kwa wanawake, hii ni filamu ambayo unapaswa au ulipaswa kuangalia wakati ukiwa kijana mdogo, kasha uiangalie tena unapofikisha miaka 30 na zaidi.

Little Miss Sunshine (2004)

Harry Potter (2001-2011)

Harry Potter imenifunza kwamba tunaweza tukapitia manyanyaso lakini tukaibuka mwishoni tukiwa imara zaidi. Pia, kupitia hii utajifunza kuwa maarifa ni silaha, na kuwa unaweza ukapita njia yako mwenye na ukawa sahihi, na si lazima ukafanya kama kila mtu anavyofanya.

Girl, Interrupted (1999)

Filamu hii ni muhimu sana hasa kwa afya ya akili kwa wanawake. Inakutia moyo na kuweza kujiona kwamba na wewe unaweza.

The Boat that Rocked (2009)

Moja kati ya filamu bora za kuchekesha nilizowahi kuziona, na pia muziki wake upo mahali pake.

Empire Record (1995)

Kwa umuhimu wa kulitafuta kabila lako.

The Craft (1996)

Unakumbuka zile stori za masuala ya ushirikina wakati ukiwa mdogo. Kama hukuwahi kusikia, nina wasiwasi na marafiki uliokuwa nao.

Almost Famous (2000)

Wakati mwingine stori unayokutana nayo, siyo uliyokuwa ukiitafuta

G.I. Jane (1997)

Simama katika kile unachokiamini, na kamwe usije ukathubutu kujisaliti.

Nights and Weekends (2008)

Onyo muhimu kati uhusiano wa kimapenzi.

Good Vibration (2012)

JIfunze kujaribu na kufanya kile ambacho kinakupendeza

Good Will Hunting (1997)

Inavunja na kutia moyo wakati huo huo. Jifunze namna ya kukabiliana na masuala yako ya kihisia ukiwa kijana, ili kujihakikisha usalama kadiri umri wako unavyosonga.

The Perks of Being Wallflower (2012)

Ni moja kati ya filamu ambazo nashauri kila mtu ambayo ndio anaingia miaka ishirini na kuendelea aiangalie. Pia, unaweza ukasoma kitabu chake kwa uelewa zaidi.

Love Story (1970)

Kila kitu kwenye filamu hii, licha ya kuwa ya zamani, kiko mahali pake. Jifunze mengi hasa yaliyotokea kipindi ambacho wewe hukuwa na ufahamu wa kuelewa kilichokuwa kikiendelea.

Toy Story 1, 2 na 3 (1995- 2010)

Kama utakuwa hujaangalia filamu hizi hadi unafikisha miaka 30, sasa utakuwa upo hai ili kufanya nini hasa?

Send this to a friend