Fiyao: Uchumi wa Tanzania unakua kwenye makaratasi au mifukoni?

0
45

Mbunge wa Viti Maalum, Stella Fiyao ameitaka Serikali kuwafafanulia Watanzania wanamaanisha nini wanaposema kwamba uchumi wa Tanzania umekua kwa sababu hali mitaani ni ngumu hata kwa wananchi kupata mlo.

Akichangia mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/2024 bungeni jijini Dodoma amesema kuwa hali za Watanzania ni mbaya, hivyo wanaposikia kuwa uchumi umekua hawaelewi unakua kwa namna gani.

Nchi 6 Afrika zinazotarajiwa kuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu 2050

“Watanzania wanajiuliza, huo uchumi unakua kwa namna gani, kwenye makaratasi au mifukoni kwako?” amehoji Fiyao akiongeza “sasa hivi hata Mtanzania aliyekuwa na uwezo wa kula milo mitatu, sasa hivi hata kula mlo mmoja ni shida.”

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Fedha na Mipango, uchumi wa Tanzania umeendelea kukua ambapo katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2022 (Januari hadi Juni), uchumi ulikua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 4.4 katika kipindi kama hicho mwaka 2021.

Wakati huo huo, mfumuko wa bei za bidhaa kwa Oktoba 2022 nao umekua kufikia 4.9% kutoka 4.8% Septemba 2022. Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kunapunguza uwezo wa wananchi kununua bidhaa na kushusha thamani ya fedha.

Send this to a friend