Flaviana Matata aelezea kuvunjika ndoa yake na mitandao ya kijamii ilivyomshambulia

0
116

Mwanamitindo kutoka Tanzania, Flaviana Matata amesema kuwa mitandao ya kijamii ni moja ya sababu zinazopelekea watu kukaa kwenye uhusiano au ndoa zenye maumivu na manyanyaso wakihofia kusemwa au kuonekana wakosaji pindi wakivunja uhusiano au ndoa.

Amezungumzia hayo na  kugusia ndo yake iliyovunjika mwaka 2019 akichangia mjadala kuhusu mahojiano ya mwanamuziki Adele ambaye alizungumza kuhusu talaka yale.

“Hakuna mtu anayeolewa ili atalakiwe. Nikizungumzia upande wangu binafsi, mimi a Deo [aliyekuwa mume wake] tulipeana talaka mwaka 2019 na intaneti haikuniacha nikae kwa amani, ilikuwa ni kana kwamba nimeua mtu,” amesema Matata (tafsiri ya mwandishi).

Licha ya changamoto alizopitia ambapo amesema ulikuwa ni wakati mgumu sana kwake, amewashukuru wale wote waliokuwa karibu nae kumfariji.

“Hatumsaidii yeyote kwa kumchafu fulani wakati ndoa inapovunjika, na hii ni sababu watu wanaendelea kubaki kwenye ndoa zenye manyanyaso na maumivu,” ameongeza.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Flaviana Matata (@flavianamatata)

Amewataka watu kabla ya kumsema mtu kwa ndoa kuvunjika, wafahamu kwanza nini kilitokea mpaka kufikia ndoa kuvunjika.

Flaviana Matata na Deogratius Massawe walifunga ndoa Agosti 2015 jijini Dar es Salaam, ndoa iliyodumu kwa miaka minne.

Send this to a friend