Flyover ya Chang’ombe yaanza kutumika leo

0
40

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imeruhusu magari kupita katika barabara ya juu (Flyover) ya makutano ya Barabara ya Chang’ombe na Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia leo Mei 30, 2022.

Profesa Mbarawa amesema kuanza kutumika kwa barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari ambao umekuwa ukijitokeza na kuleta usumbufu kwa wananchi.

Aidha, ametoa agizo kwa wakandarasi kuwa, kufikia Oktoba mwaka huu barabara zote mbili za flyover katika eneo hilo ziwe zimekamilika na kuanza kutumika mara moja.

Send this to a friend