Fundi simu jela miaka 14 kwa kusambaza picha za utupu

0
122

Kijana mmoja (22) nchini Ghana amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya kusambaza picha za uchi za mwanamke wa Lebanon kwenye mitandao ya kijamii bila hiari yake.

Solomon Doga ambaye ni fundi simu amehukumiwa na mahakama katika kitongoji cha Adenta huko Accra, baada ya kukiri mashtaka hayo ambapo alimtaka mwanamke huyo amlipe kiasi cha fedha ambacho hakikutambuliwa vinginevyo atasambaza picha zake, lakini hakufanya hivyo.

Aidha, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali, Inspekta Maxwell Lanyo ameiambia mahakama kuwa kijana huyo alifungua simu ya mwanamke huyo wa Lebanon anayeishi Accra na kisha kuchukua picha zake kinyume cha sheria.

Raia wa China anayewakaririsha na kuwarekodi watoto nyimbo za ubaguzi akamatwa

Baadaye mshtakiwa alichapisha picha za mwanamke huyo akiwa mtupu kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha kukamatwa kwake na kisha kufungwa jela.

Sheria mpya za usalama wa mitandao za Ghana zilizoletwa miaka miwili iliyopita, zimekataza uchapishaji wa picha za utupu, ambapo adhabu yake ni kifungo cha kati ya miaka mitano na 25 jela.