Fursa 6 za kibiashara zinazoweza kukupa utajiri

0
15

Afrika ni bara lililojaa fursa nyingi za biashara zinazoendeshwa na rasilimali zilizopo, teknolojia na masoko makubwa. Hakika kuna nafasi kwa mamilionea zaidi kuibuka barani Afrika kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana.

Kulingana na Business Insider Afrika, hizi ni fursa 6 za biashara zinazoweza kukupa utajiri barani Afrika.

Vyombo vya Habari na Burudani
Vyombo vya habari na burudani vinaweza kutengeneza kundi la mamilionea kwa kuwa tasnia ya habari, muziki na filamu Afrika imekuwa ikipokea wafuasi wengi ndani na nje ya bara hili.

Faida 5 za kulia usizozijua

Chakula na Biashara ya Kilimo
Biashara hii ina faida kubwa barani Afrika pamoja na fursa za biashara zisizoisha. Wajasiriamali walio na rasilimali na ujuzi wa kuzalisha chakula ndani ya nchi wanaweza kuingiza faida nyingi endapo watatumia mbinu bora na za kisasa.

Biashara za Rejareja
Kwa ukuaji wa haraka wa miji na tabaka la kati linaloongezeka, Waafrika wanakuza uchumi wao kupitia masoko ya rejareja. Gabon, Tanzania, Namibia, Nigeria, na Rwanda ni nchi za Kiafrika zenye fursa nzuri za biashara katika soko la reja reja.

Mitindo na Urembo
Sekta hii inapanuka na kuwa na idadi kubwa ya vijana barani Afrika. Nigeria inaongoza kutokana na idadi kubwa ya watu inayotarajiwa kuongezeka zaidi ifikapo mwaka wa 2050, tasnia hiyo inaweza kutengeneza mamilionea.

Majengo
Upungufu wa nyumba ni tatizo barani Afrika, na kuziba pengo kunaweza kukufanya kuwa milionea. Fikiria endapo una uwezo mzuri wa kujenga nafasi za ofisi na nyumba zenye kipato cha chini kwa kukodisha au kuuza.

Mtandao na Teknolojia
Matumizi ya mtandao barani Afrika na ushiriki wa teknolojia yanaongezeka, tasnia ya mtandao na teknolojia barani Afrika inatoa fursa nzuri za biashara kwa wafanyabiashara na wavumbuzi. Waafrika wenye ujuzi wanaweza kuwa mamilionea na uvumbuzi kwa kutatua changamoto na matatizo na teknolojia.

Send this to a friend