Gari la ofisi ya Mkuu wa Mkoa lakamatwa na bidhaa za magendo

0
59

Operesheni maalum iliyoundwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe imefanikiwa kukamata magari 14 yenye bidhaa za magendo na moja wapo likiwa ni gari ya ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amesema kati ya magari 14 yaliyokamatwa, gari moja linatokea ofisini kwake na lingine ni gari ambalo limekuwa likitafutwa kwa miaka mingi.

“Bidhaa za magendo zilizokamatwa ni vitenge, pombe kali, vipodozi vikali vilivyozuiliwa kwa mujibu wa sheria zetu, vipo vifaa vya shule na maofisini, mayai, vinywaji na bidhaa za kula,” alisema Mgumba

Aidha, amesema bidhaa hizo zina gharama ya zaidi ya TZS milioni 180 na tayari madereva wote 14 wanashikiliwa na polisi pamoja na magari yao, huku waliokimbia kuendelea kutafutwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kuanzia sasa mmiliki wa gari atapigwa faini kwa kosa la gari lake kubeba magendo pamoja na kusaidia kumpata dereva wake ili dereva naye ataje mtu aliyepakia mzigo wa magendo.

Send this to a friend