Gari la TFF hatarini kupigwa mnada ili kulipa deni

0
89

Wakili wa taasisi za Filbert Bayi, Karoli Tarimo amefungua maombi akiiomba mahakama iruhusu kulikamata basi la TFF ili kulipa deni la TZS 56,446,700.

Inadaiwa kuwa taasisi hiyo inaidai TFF fedha hizo kwa miaka mitatu ambapo kwa mujibu wa Tarimo zilikuwa ni gharama ya kambi kwa timu za vijana wa miaka 13, 15, 17 na ile ya wanawake Kibaha mkoani Pwani.

TFF yamjibu Manara

Alisema Juni 3, mwaka huu taasisi hiyo iliingia makubalino na TFF ya miaka mitatu kutoa huduma za viwanja, usafiri, kambi na chakula wenye thamani ya TZS milioni 521.4 ambazo walikubaliana zilipwe kwa awamu na kusalia na TZS milioni 76.4 ambazo Julai 20, mwaka jana Rais wa TFF, Wallace Karia alikiri kuwa suala hilo lilikuwa linashughulikiwa.

Hata hivyo, Tarimo amesema baada ya TFF kutoonesha dalili za kulipa ndani ya makubalino walifungua kesi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na TFF ilikubali kudaiwa na kuahidi kulipa kwa awamu kuanzia Novemba, 2021 hadi Aprili 2022. Hata hivyo tangu ilipe awamu mbili haijalipa tena.

“Mei 17 tulifaili maombi kukazia hukumu kuomba kukamatwa gari la TFF na kuliuza. Maombi yamesikilizwa Julai 21 na shauri limeahirishwa hadi Agosti 4,” amesema.

Send this to a friend