Gari lililoibwa kwenye mradi wa SGR lakamatwa likitafutiwa mteja

0
30

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limekamata gari aina ya HOWO tani 12 lenye thamani ya TZS milioni 180 liliokuwa limeibwa katika mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) likiwa katika harakati za kutafutiwa mteja ili liuzwe mkoani Tabora.

Katika taarifa yake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda ameeleza kuwa gari hilo ambalo ni mali ya Kampuni ya ujenzi ya CCECC ilikamatwa Mabama wilaya ya Urambo.

“Ilipotea Januari 27, 2023 katika Kambi ya Malampaka ikapatikana Januari 29, 2023 ikiwa inapelekwa kwa mnunuzi, katika hali ya kawaida gari haliwezi kutoka ndani ya fensi ikapotea maana yake kuna watu wa ndani wameshirikiana na walinzi kuhakikisha kwamba gari linatoka,” amesema Chatanda.

Amesema katika operesheni iliyokuwa inafanyika katika mradi wa ujenzi wa reli ya SGR, jumla ya watuhumiwa saba walikamatwa wakiwa na vifaa mbalimbali vya ujenzi vilivyoibiwa katika mradi huo.

Kamanda Chatanda ametaja baadhi ya vitu vilivyokamatwa kuwa ni mafuta lita 560, pikipiki 8 zilizokuwa zinatumika kubebea mafuta, mifuko ya saruji 79, mirija ya kunyonyea mafuta 21, baiskeli 8, na mabomba ya chuma 19.

Send this to a friend