Gazeti la Uhuru lamlisha maneno Samia urais 2025

0
44

Chama kinachotawala nchini Tanzania (Chama cha Mapinduzi-CCM) kimekanusha taarifa ya gazeti linalomilikiwa na chama hizo, la Uhuru yenye kichwa cha habari “Sina wazo kuwania Urais 2025 – Samia”.

CCM imesema imesikitishwa na upotoshaji uliofanywa na gazeti hilo toleo la Agosti 11, 2021 na imesisitiza kuwa wahusika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

“Huu ni upotoshaji mkubwa wa kumlisha maneno Rais Samia Suluhu Hassan,” ameeleza Katibu wa NEC wa CCM, Shaka Hamdu Shaka katika taarifa iliyotolewa na chama hicho.

Gazeti hilo limeandika taarifa hiyo likieleza kuwa ni moja ya mambo ambayo Rais Samia Suluhu Hassan aliyeweka wazi wakati wa mahojiano yake na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

CCM imewataka wanachama wake na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo kwani imeandikwa na watu wenye maslahi binafsi.

Send this to a friend