Geita: Auawa na wasiojulikana kisha kukatwa kiganja

0
66

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Milembe Seleman (43) mkazi wa mtaa wa Mseto ameuawa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Mwatulole, Kata ya Buhalahala, Geita Mjini mkoani Geita.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi Berthaneema Mlay amesema tukio hilo limetokea leo Aprili 26, saa moja asubuhi.

Mlay amesema baada ya Jeshi la Polisi kufika katika eneo hilo, wamekuta mwili wa marehemu umekatwa sehemu mbalimbali ikiwemo kichwani, usoni pamoja na mikono yote miwili huku mkono wa kulia ukiondolewa kiganja.

Kamanda Mlay amesema mpaka sasa watu wanne wanashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, huku mwili huo ukihifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema wameamka asubuhi na kukuta mwili huo ukiwa umetelekezwa katika jengo ambao linadaiwa lilikuwa likimilikiwa na marehemu huyo.

Send this to a friend