Geita Gold yamalizana na FIFA

0
83

Uongozi wa klabu ya soka ya Geita Gold imetoa taarifa kwa mashabiki, wadau na wanamichezo kuwa tayari imemalizana na adhabu iliyotolewa na FIFA  juu ya kufungiwa kufanya usajili.

Klabu imesema tayari imetekeleza matakwa yote ya kisheria na kikanuni kwa kuzingatia miongozo ya shirikisho la mpira wa miguu FIFA, na sasa ipo huru kuendelea na utendaji wake.

Aidha klabu hiyo imesema imejipanga kufanya vizuri katika msimu wa mashindano 2022/23 ili kuendeleza hali ya ushindani katika michuano ya ndani na kimataifa.

Juni 24 mwaka huu, Geita Gold ilifungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu d
Duniani (FIFA)  kufanya usajili hadi itakapomlipa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Ettiene Ndayiragije baada ya kudai kuvunjiwa mkataba na klabu hiyo.