Geita: Mtoto aliyechomwa mikono na mama yake kisa wizi aeleza ukweli

0
80

Mwanafunzi aliyekuwa anasoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Shahende, Kata ya Butobela, wilaya ya Geita mkoani Geita, Helena Paul (13) aliyechomwa moto mikono na mama yake mzazi kwa tuhuma za kumuibia TZS 30,000 amesema mama yao aliwachoma mikono yeye na mdogo wake wa kiume, Junior Bahati Paul  kwa madai ya kumuibia kiasi hicho cha pesa.

”Mama alisema amepoteza pesa, mdogo wangu akamwambia mama zote umezichukua wewe mama akasema mnauhakika gani nimezichukua zote hela. Akatoka nje mama akafata manyasi akaja akatufunga kamba mikono zote akatufunga na nyasi  akawasha na moto akamaliza akachukua fimbo akaanza kutupiga,” amesema.

Mtendaji wa Kijiji cha Shahende, Edar Michael amesema  baada ya kupata taarifa za tukio hilo walichukua hatua za kumkamata mtuhumiwa wa tukio hilo  na kumfikisha katika kituo cha polisi baada ya kuhojiwa mama huyo alidai watoto hao walimuibia TZS 30,000.

“Baada ya kufika na kumkuta huyo mama tukawa tumemchukua baada ya kumhoji alidai kwamba hawa watoto wamechukua hela kiasi cha shilingi 30,000. Baada ya kuwaadhibu hao watoto hawakuweza kusema ukweli  ndo akachukua jukumu la kuwachoma mikono ili waeleze ule ukweli” amesema mtendaji wa kijiji.

Send this to a friend